Papa afanya misa ya mwisho kabla kujiuzulu

Image caption Papa amesema anaelewa uzito wa uamuzi wake

Papa Benedict amefanya misa yake ya mwisho hadharani kabla ya kujiuzulu rasmi hapo kesho, kitendo kama hicho kilifanyika katika Kanisa Katoliki miaka mia sita ilyopita.

Amewaambia maelfu ya watu waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro huko Vatican kwamba alikuwa anafahamu uzito wa aamuzi wake lakini amefarijika kutokana na imani yake kwa ungu na Kanisa Katoliki.

Papa aliwaambia mamia ya waumini waliofika kushuhudia misa yake kuwa anafahamu vyema athari za umauzi wake lakini alikuwa na amani kwa sababu ya imani yake kwa Mungu na kanisa.

Mara kwa amara waumini walishangilia hotuba zake akisema kuwa alihisi kupotewa na nguvu katika miezi ya karibuni na kumtaka Mungu kumsaidia katika kufanya uamuzi huu.

Pia alisema kuwa atamuombea mrithi wake atakayechaguliwa katika wiki chache zijazo.