Siku ya mwisho ya Papa Benedict wa 16

Image caption Papa ameahidi kumheshimu mrithi wake

Papa Benedict amewaambia makadinali kadhaa kwamba atamuheshimu na kumtii mrithi wake.

Kiongozi huyo alikutana na baadhi ya makadinali wakati ambapo amefika ukingoni mwa uongozi wake katika kanisa katoliki baada ya kuamua kujiuzulu.

Papa Benedict amesema anatarajia kuwa Mungu atawaongoza na kuwalelekeza kuhusu nani hasa anastahili kuwa mrithi wake.

Baadaye kila kadinali aliyekuwepo mahali pale alimbusu Papa Benedict mkononi kama ishara ya kumuaga