Makadinali wakutana kumchagua papa

Image caption Makadinali wa Kikatoliki

Makadinali wa Kanisa Katoliki kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Roma kuanza mkutano wa awali wa faragha wa kumchagua mrithi wa Papa Benedict XVI.

Mkutano huo utaamua tarehe ya kuanza utaratibu wa mfululizo wa kura za siri. Makadinali hao watafanya mikutano ya kila siku hadi hapo papa mpya atachaguliwa.

Wahandisi wa ufundi wa teknolojia ya mawasiliano watakuwa wakiwachunguza makadinali, na simu zao zitapigwa marufuku wakati wa shughuli hiyo.

Uchaguzi huu unfanywa baada ya Papa Benedict XVI kujiuzulu baada ya miaka minane ya kuwaongoza Wakatoliki bilioni 1.2.

Ni papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600.