Zimbabwe haitaki waangalizi wa Ulaya

Image caption Rais Robert Mugabe na Waziri mkuu Morgan Tsvangirai

Maafisa nchini Zimbabwe wanasema hawatakaribisha makundi ya waangalizi kutoka nchi za magharibi kuchunguza kura ya maoni kuhusu katiba ama uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Simbarashe Mumbe-ngegwi amesema wachunguzi wa nchi za magharibi hawatakuwa na malengo kwa sababu muungano wa ulaya na Marekani waliweka vikwazo dhidi ya rais Robert Mugabe na maafisa wengine kutoka chama chake cha ZANU PF.

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itapunguza madaraka ya rais itafanyika Jumamosi.

Wachunguzi kutoka Afrika wamealikwa kufuatilia uchaguzi huo.