Tisho la UN kuhusu wanajeshi wabakaji DRC

Image caption Wanawake waathiriwa wa ubakaji DRC

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya wanajeshi wanaoshukiwa kufanya ubakaji nchini humo.

Ujumbe wa umoja huo nchini Congo umesema kuwa utasitisha ushirika wake na vikosi viwili mahsusi vya kijeshi vilivyoshukiwa kuhusika iwapo hatua haitachukuliwa katika mwezi mmoja.

Hii imetokea huku wanawake duniani wakiadhimisha hii leo siku ya wanawake duniani.

Wanawake wengi wa eneo la maziwa makuu wameathiriwa na vita na hata hukosa huduma muhimu ya afya.