Kesi dhidi ya William Ruto yaakhirishwa

Image caption William Ruto akipiga kura yake katika uchaguzi wa Kenya

Mahakama ya kimataifa ya ICC imeakhirisha kesi ya mshukiwa wa uhalifu wa kivita nchini Kenya, William Ruto ambaye pia ni mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta anayewania urais.

Kesi dhidi ya Ruto sasa itasikilizwa,katika mahakama ya ICC, tarehe 28 mwezi Mei baada ya mawakili wake kulalamika kuwa hawakuwa na muda wa kutosha kujiandaa kwa utetezi.

Ruto, anakabiliwa na kosa la kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu elfu moja waliuawa na maelfu kuachwa bila makao.

Hayo yalitokea kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata na kusababisha vurugu. Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo alisema ni muhimu kwa washukiwa kujiandaa

Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta nayo iliakhirishwa na sasa itasikilizwa mwezi Julai.