Oscar Pisorius anaelekea kukata tamaa

Image caption Oscar Pistorius anakana madai ya kumuua mpenzi wake Reeva

Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, anayetuhumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake, huenda akajinyonga, rafiki wa karibu wa familia yake ameambia BBC.

Mwanariadha huyo, amejipata pabaya baada ya kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ili kugharamia kesi yake, alisema Mike Azzie.

Bwana Azzie alitoa matamshi yake katika kipindi cha BBC, kuhusu kesi inayomkabili Pistorius, ambapo mwanariadha huyo anakanusha madai hayo.

Wakati huouo, mawakili wa mwanariadha huyo , wameomba mahakama kulegeza vikwazo vya dhamana aliyopewa.

Bwana Pistorius, ambaye anakabiliwa na kesi kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi jana, anakanusha madai kuwa alipanga kumuua Reeva akisema hakujua kama ni yeye wakati wa kitendo hicho.

Aliachiliwa kwa dhamana tarehe 22 mwezi Februari na kesi itasikilizwa tena mwezi Juni.

Bwana Azzie, ambaye amekuwa akiwasiliana na Pistorius, alisema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali yake ya kiakili

Azzie, ambaye Oscar humuiya mjomba, Mike, alisema kuwa manariadha huyo, amelazimika kuuza farasi wake ili kugharamia kesi yake.

''Hajiamini hata kidogo na ni kama tu ambaye anazunguka zunguka asijue anakokwenda,'' alisema bwana Azzie

"naweza kusema kwa kuongea naye tu, anaonekana kama mtu aliyevunjika moyo sana. Naweza kusema anakaa kama mtu ambaye amekata tamaa na hata anaweza kujinyonga . Na hiyo inatia wasiwasi mkubwa,'' alisema Azzie katika kipindi maalum kuhusu Oscar.