Mauaji ya halaiki nchini Syria

Image caption Idadi ya wakimbizi wa Syria pia imeelezewa kuongezeka kutokana na vita

Umoja wa mataifa umesema kuwa umepokea ushahidi wa mauaji ya halaiki na uharibifu wa mitaa nchini Syria.

Katika ripoti mpya, wachunguzi wa uhalifu wa kibinadamu wanatuhumu pande zote mbili serikali na upinzani kwa kuhujumu maisha ya watu kote nchini humo.

Wanatoa mfano wa matukio matatu ya mauaji ya halaiki katika mji wa Homs, ambako umoja wa mataifa unasema kuwa wafungwa hamsini waliuawa na majeshi ya serikali na huku familia za watu zikiuawa majumbani kwao.