Papa Mpya ateuliwa kuongoza Watoliki

Image caption Moshi muepe, Papa mpya!

Hatimae Kanisa katoliki limempata kiongozi mpya atakaye chukuwa mahali Papa Benedict aliyejiuzuli.

Papa Mpya alichaguliwa katika duru ya tano ya upigaji kura uliofanywa na makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.

Kwa wakati huu mbali na maelfu ya watu waliokusanyika eneo la St. Peters huko Vatican dunia nzima wanasubiri kujua jina la Papa mpya na ataamua kuchukuwa jina gani la Ki-Papa.