Kijana aliyejichoma moto afariki Tunisia

Image caption ramani ya Tunisia

Mtu mmoja aliyejichoma moto mjini Tunis amefariki kutokana na majeraha yake. Daktari aliyekuwa akimhudumia Adel Khadri amesema kuwa alifariki mapema Jumatano asubuhi.

Bwana Khadri alijichoma moto katika mji mkuu wa Tunis siku ya Jumanne akilalamikia ukosefu wa ajira. Alikuwa akiiga mfano wa mtu mwingine Mohamed Bouaziz aliyejiua na kusababisha mzozo mkubwa ulioleta mageuzi ya mataifa ya arabia miaka miwili iliyopita.

kifo chake sasa kinatokea huku Tunisia ikizongwa na malumbano ya kisiasa kufuatia kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa upinzani. Bunge la nchi limeidhinisha hivi punde serikali mpya inayonuiwa kutuliza hamaki katika kura ya kuwa na imani na rais.