Wanachama wa MDC wakamatwa Zimbabwe

Bwana Tsvangirai na Rais Mugabe

Chama cha waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, kinasema kuwa Jumapili asubuhi polisi waliwakamata wanachama wake watatu waandamizi kutoka majumbani mwao.

Chama cha Bwana Tsvangirai, MDC, ambacho zamani kilikuwa upinzani, kinasema hakuna sababu iliyotolewa kwa maafisa wake kukamatwa.

Wakili mashuhuri wa kutetea haki za kibinaadamu, Beatrice Mtetwa, piya inaarifiwa kuwa amezuwiliwa ili kuhojiwa.

Afisa wa MDC alikamatwa Jumamosi kabla ya upigaji kura ya maoni kuanza kuhusu katiba mpya.

Vyama vyote vinaunga mkono katiba iliyopendekezwa, lakini baadhi ya makundi ya kutetea haki za kibinaadamu yameipinga.