Rais Obama awasili nchini Israel

Rais Obama
Image caption Rais Obama

Rais Barack Obama amewasili nchini Israel. Hii ni ziara yake ya kwanza kama rais wa Marekani.

Huku akiwasili, waandamanaji walikusanyika na ulinzi kuimarishwa nchini Israel na katika maeneo ya Palestina.

Bwana Obama anategemewa kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa ziara yake ya siku tatu.

Vita nchini Syria na wasiwasi kuhusu nia za Iran za kinyuklia ni kati ya maswala muhimu, wanasema waandishi habari.