Rais wa China kuzuru Urusi

Rais Xi Jinping
Image caption Rais Xi Jinping

Rais wa China anaelekea Urusi katika ziara yake ya kwanza ng’ambo itakayompeleka pia Tanzania, Afrika Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akiwa Urusi, anategemea kukutana na Rais Vladimir Putin, na inakisiwa kwamba watajadili maswala ya nishati na uwekezaji.

Akiongea kabla ya kuondoka, Bwana Xi alisema kuwa nchi hizo mbili "zilikuwa na uhusiano muhimu wa kimkakati" na kwamba wanaongea "lugha moja ".

Akiwa Afrika Kusini, atahudhuria mkutano wa tano wa Brics utakaofanyika mnamo 26-27 Machi. Brics inajumuisha nchi za Brazil, Urusi, India, China and Afrika Kusini – nchi tano muhimu zinazozidi kukua kiuchumi.

Uchina ndiyo nchi inayofanya biashara nyingi zaidi na Afrika, kuliko Marekani na Ulaya.

"Uhusiano kati ya Uchina na Afrika ni wa kina," Bwana Xi alisema.

Xi Jinping alithibitishwa kuwa rais wiki iliyopita.