San Su Kyi ahudhuria sherehe za kijeshi

Image caption Su Kyi alifungwa kifungo cha nyumbani kwa miaka mingi kwa kupinga serikali Burma

Kiongozi wa upinzani nchini Burma, Aung San Su Kyi, amehudhuria sherehe ya kijeshi kwa mara ya kwanza, tangu aachiliwe kifungo cha nyumbani, ikiwa ishara kamili kuwa uhusiano wake na viongozi wa kijeshi unazidi kuimarika.

Aliketi katika mstari wa mbele wakati aliyekuwa kamanda wa jeshi wa taifa hilo akisema kwamba jeshi litaendelea kutekeleza wajibu muhimu katika Serikali ya Taifa hilo.

Alisema uhusiano huo utaimarisha taifa kidemokrasia. Jeshi kwa wakati huu linaendelea kusaidia kukabiliana na mapigano kati ya Waislamu na Wabudha.

Waislamu wameshambuliwa mara kwa mara.