Waliokufa Dar-es-salaam wafika 18

Wakuu wa Tanzania wanasema sasa inajulikana kuwa watu 18 walikufa wakati jengo moja lilokuwa likijengwa lilipoporomoka mjini Dar es Salaam.

Watoto wawili ni kati ya maiti zilizopatikana.

Kazi ya uokozi inaendelea lakini hakuna matumaini ya kunusuru maisha.

Watu kadha bado wametoweka.

Jengo hilo la ghorofa kadha lilikuwa kati-kati ya mji.

Waandishi wa habari wanasema ujenzi wa majumba umeongezeka Tanzania kwa sababu ya uchumi kukuwa, lakini kuna wasi-wasi kuwa vigezo vya ujenzi havifuatwi.