Waandamana baada ya kula chakula chenye sumu

Image caption Chuo kikuu cha Al AzHar

Wanafunzi katika chuo kikuu mashuhuri cha Al Azhar nchini Misri, wanapanga kuandamana baada ya takriban wenzao miatano kugonjeka baada ya kula chakula kibaya.

Siku ya Jumatatu mamia ya wanafunzi hao waliandamana nje ya kumbi za wanafunzi wakitaka mkuu wa chuo hicho ajiuzulu.

Chuo hicho kinamilikiwa na mamlaka ya msikiti wa Al Azhar, inayotazamiwa kuwa mamlaka kuu ya waisilamu wa Sunni nchini humo.

Maafisa wa utawala nchini humo wameagiza uchunguzi kufanywa.