Mazungumzo na Iran yaendelea

Wapatanishi wa kimataifa wamerejea kwenye mazungumzo na Iran kuhusu namna ya kuzuwia mradi wa nuklia wa nchi hiyo.

Siku ya kwanza ya mazungumzo haikufikia mapatano.

Waakilishi wa Iran wanasema wameeleza kwa ufupi mapendekezo yao muhimu kwenye mazungumzo hayo yanayofanwa Kazakhstan.

Lakini mwanabalozi mmoja kutoka mataifa ya magharibi alisema Iran haikutoa jawabu thabiti kuhusu mapendekezo ya karibuni ya mataifa makuu pamoja na Marekani, Urusi na Uingereza.

Mataifa hayo yanasema yatapunguza baadhi ya vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, iwapo nchi hiyo itaacha sehemu fulani za mradi wake wa nuklia.

Mwandishi wa BBC kwenye mazungumzo hayo anasema inaonesha pande hizo mbili kama hazifanyi mazungumzo kwa sababu maneno yao yanapishana.