Mandela atoka hospitali

Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ameruhusiwa kutoka hospitali ambako akitibiwa homa ya mapafu yaani pneumonia kwa siku kumi.

Serikali imetoa taarifa kusema kuwa hali ya Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, imetengenea sana na ataendelea kutibiwa nyumbani.

Hali ya Bwana Mandela ilishtusha mwezi Disemba mwaka jana ambapo alilazwa hospitali kwa karibu majuma matatu kwa sababu ya ugonjwa wa mapafu na kijiwe kwenye nyongo.

Rais Zuma aliwashukuru matabibu na wauguzi kwa jitihada yao ya kumuungalia Bwana Mandela kwa uzuri.