Dunia ijibu Korea Kaskazini kwa umoja

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Uingereza, William Hague, anasema kuhusu msukosuko wa Korea Kaskazini wa hivi sasa, ulimwengu unafaa kujibu kwa umoja, utulivu na uwazi.

Bwana Hague ameiambia BBC kwamba ulimwengu unafaa kuwa na wasiwasi kuhusu shughuli za kinuklia za Korea Kaskazini lakini uepuke kujibu kila tamshi kali linalotoka Pyongyang.

Matamshi ya Bwana Haig yanafuatia taarifa kwamba Marekani imeakhirisha majaribio ya kombora la masafa marefu huku mvutano ukizidi na Korea Kaskazini.

Jaribio hilo la kawaida, lilipangwa kufanywa kwenye kambi ya jeshi la wanahewa katika jimbo la California.

Kwa mujibu wa afisa wa Wizara ya Ulinzi Marekani inataka kuepukana na wazo kwamba inachochea zaidi msukosuko wa hivi sasa na Korea Kaskazini.

Jaribio sasa limeakhirishwa hadi mwezi ujao.