Kerry azuru Uturuki

John Kerry

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, anazuru Uturuki katika safari ambapo piya atakwenda Israil, Ufukwe wa Magharibi pamoja na London na mashariki mwa Asia.

Bwana Kerry anazuru Istanbul wiki mbili baada ya kusaidia kuleta makubaliano ya mapatano baina ya Uturuki na Israil.

Uhusiano baina ya nchi mbili hizo uliharibika baada ya Israil kuvamia meli za Uturuki zilizokuwa zikielekea Gaza mwaka wa 2010.

Wakati wa ziara yake nchini Uturuki Bwana Kerry anatarajiwa kuzungumza na Waziri Mkuu, Recep Tayyip Erdogan, kuhusu vita vya nchi jirani, yaani Syria.