Margaret Thatcher afariki dunia

Image caption Margaret Thatcher

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher ameaga dunia.

Thatcher alikuwa na umri wa miaka 87 na msemaji wake ameelezea kuwa alifariki kutokana na ugonjwa wa kiharusi

Thatcher alikuwa mwanamke wa kwanza waziri mkuu wa Uingereza na anasemekana kuleta mageuzi makubwa kisiasa Uingereza alipochukua mamlaka mwaka 1979.

Pia alisifika sana na kuwa mwanamke mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Uingereza.