Mfululizo wa mashambulizi nchini Iraq

Image caption Mashambulizi pia yalitokea katika mji wa Nassiriya

Umetokea mfululizo wa mashambulio ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari , katika miji kadhaa nchini Iraq asubuhi ya leo , wakati watu wakielekea kazini .

Mabomu hayo yamewauuwa takriban watu watano.

Watu wengi pia walijeruhiwa na idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka. Mengi kati ya masambulio hayo yameripotiwa katika mji mkuu Baghdad na mengine katika miji muhimu ukiwemo miji ya Fallujah Kirkuk.

Mashambulio hayo yamekuja siku tano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa majimbo ukiwa ni uchaguzi wa kwanza kuendeshwa na taifa hilo tangu kuondoka kwa majeshi ya marekani mnamo mwaka 2011.

Katika mashambulio ya jana mgombea mmoja aliuawa