Redio na Televisheni washirika

Vyombo Washirika wa idhaa ya kiswahili ya BBC

Redio Washirika

Ra dio Free Africa

RFA ilizinduliwa mwaka 1997 na hutangaza kote nchini Tanzania

Kiss FM Tanzania

Kiss FM ilianza kupeperusha matangazo yake mwaka 1998 na ilipoanza ilikuwa kwa lugha ya Kiingereza

West FM

Sikiliza taarifa kuhusu Magharibi ya Kenya kupitia masafa ya 94.9 na 104.1 FM ukiwa eneo hilo na sehemu za Mashariki ya Uganda pamoja na Jimbo la Siaya

Radio One

Radio One ni moja ya stesheni za mwanzo kuvuma nchini Tanzania na yenye kusikika kwa masafa ya FM ikipeperusha kwa masaa 24 kila siku

Pamoja FM

Pamoja FM ni stesheni ya kijamii ambayo inapeperushia matangazo yake katika mtaa wa mabanda wa Kibera mjini Nairobi

Star FM

STAR FM ndio kituo cha kwanza kuanza kupeperusha matangazo yake Kaskazini mwa Kenya na katika baadhi ya maeneo ya Somalia

Nenah FM

'The Voice of Transformation' au Sauti ya mabadiliko ni kituo binafsi. Kilianzishwa tarehe sita Oktoba mwaka 2008. Kituo hicho hupeperusha matangazo yake kwa lugha za Ngakarimojong, Kiingereza, Kiswahili, Pokot, Ethur na Ateso.

KU 99.9 FM

Radio ya chuo kikuu cha Kenyatta, (KU 99.9 FM), ni stesheni ya kijamii na hupeperusha vipindi vya kuvutia ambavyo hugusia maisha ya kaiwaida ya chuoi.

Radio Busoga 96 FM Log

Busoga 96 fm ilizinduliwa mwaka 2001 kama kituo cha kwanza cha redio Mashariki ya Uganda.

Zenji 96.8 FM

Zenji 96.8 FM ni redio ya kwanza ya binafsi kuanza kupeperusha matangazo yake visiwani Zanzibar. Ilizinduliwa tarehe 8 mwezi Julai mwaka 2005. Ndio stesheni mashuhuri sana ya redio visiwani Zanzibar.

Stesheni inayopeperusha matangazo yake kutoka Arusha na inaweza kusikika kwa masafa ya 105.7 fm mjini humo, MBEYA 93.8fm, MORO 94.8fm, MWANZA 92.5fm, DODOMA 88.6fm and TANGA 98.9FM.

Inajulikana Mashariki ya Uganda kama stesheni inayocheza muziki wa Rock. Setesheni ya Rock Mambo ni Redio ya kijamii na huwafikia watu wa mashinani nchini Uganda.

Karamoja 94.7 FM

All Karamoja 94.7 fm ilianza kutangaza kwa lengo la kuelimisha jamii , kuhabarisha na kutumbuiza watu mada yake ikiwa kilikom, maslahi ya jamii , elimu ya kisiasa na maswala ya elimu.

Radio Paidha

Redio Paidha ni stesheni yenye lengo la kuchangia maendeleo mashinani kupitia kwa vipindi vyake vya hali ya juu pamoja na ujumbe muhimu kwa wenyeji na waskilizaji wa kimataifa kwa bei nafuu.

Canal Revelation

Radio Canal Revelation (CPR), ilizinduliwa ili kutoa huduma kwa vijana uwezo wa kupata habari kuhusu afya na kuwatumbuiza watu

KBC

KBC ni stesheni ya kitaifa nchini Kenya

Bonesha FM

Ni stesheni ya kwanza yenye masafa ya FM kupeperusha matangazo ya BBC na inaweza kusikika mjini Bujumbura kwenye masafa ya 96.8 FM,Manga 102.4 FM na Inanzerwe 87.7 FM

Radio 10

Ilianzishwa mwaka 2004, Radio10 - 87.6 FM ni stesheni ya kwanza na inayosemekana kuwa nzuri zaidi ya kibinafsi nchini Rwanda

Voice of Kigezi

Voice of Kigezi (Sauti ya Kigezi) ni redio ya kibisahara inayosikika Kusini Magharibi mwa Uganda hasa kwa lugha za Rukiga, Kinyarwanda,Swahili na Kiingereza. Inawalenga hasa watu wenye umei wa kati ya miaka 16 hadi 40.

RAGA FM ni stesheni ye kibiashara nchini Congo ambayo huchanganya burudani na habari pamoja na muziki

Redio Lira 95.3 fm ilizinduliwa mwaka 1999 Kaskazini mwa Uganda

Televisheni Washirika

Star TV

Kituo cha televisheni cha Star TV, kilizinduliwa mwaka 2000 kuingia katika biashara televisheni. Kwa sasa kinawatangazia watazamaji wanaopokea stesheni za kulipiwa.

Raga TV

Kituo cha televisheni cha RAGA kilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 1997, kama kituo cha kibiashara kikiwa na lengo la kutumbuiza watazamaji wakati ikiendelea kuleta mambo mapya katika sekta ya utumbuizaji katika jamuhuri ya kidemkrasia ya Congo. Kinasifika kuwalenga vijana na kutangaza mambo yanayopendwa sana na vijana.