Msako wa mshukiwa wa mashambulizi Boston

Image caption Mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya Boston

Polisi nchini Marekani wanamsaka mshukiwa mkuu wa mashambulizi yaliyotokea katika mbio za Boston Marathon katika mji mdogo karibu na Boston.

Operesheni kubwa ya polisi inayoendelea ilianza baada ya afisaa mmoja wa polisi kuuawa katika chuo ya mafunzo anuai cha Massachusetts .

Mshukiwa mmoja aliuawa baada ya polisi kumfukuza hali iliyosababisha ufyatulianaji wa risasi umbali wa kilomita kumi kutoka Boston.

Mshukiwa mwingine ambaye picha yake ilionyeshwa alikuwa amevalia kofia huku akikimbia kutoka eneo la Watertown.

Polisi walisema kuwa wanaume hao wawili walishukiwa kumuua polisi mmoja, katika chuo hicho cha Massachusetts Jumanne jioni. Thursday.

Baadaye waliiba gari mmiliki wake akiwemo ndani kwa kutumia nguvu lakini walimwachilia mmiliki bila kumjeruhi.

Shirika la FBI limetoa picha kadhaa za washukiwa hao.

Wawili hao waliwasrushia polisi mabomu na hata kwuafyatulia risasi kabla ya kusimamishwa katika eneo la Watertown.

Wakaazi wa mtaa huo wameshauriwa kusalia makwao.