London marathon yaanza

Siku sita baada ya shambulio la bomu kwenye marathon ya mjini Boston, Marekani, marathon ya London nayo imeanza kati ya ulinzi mkubwa.

Watu waliokufa Boston walikumbukwa mjini London kwa watu kukaa kimya kwa sekunde 30 kabla ya mashindano kuanza, na wakimbiaji waliombwa wavae kitambaa cheusi.

Polisi wamesisitiza kuwa hakuna ishara ya tishio la kuunganisha mbio hizo mbili, lakini wameweka askari mamia zaidi mabarabarani ili kuthibitisha usalama wa wale wanaoshiriki.

Watu zaidi ya 30,00o wanatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo, na watazamaji nusu milioni watarajiwa kujitokeza.