Washukiwa wa Al Qaeeda wakamatwa Uhispania

Image caption Haijulikani kilichoshinikiza kukamatwa kwa washukiwa Uhispania

Polisi nchini Uhispania wamewakamata washukiwa wawili kutoka Afrika Magharibi wanaoaminika kuwa na uhusiano na kundi la al-Qaeda.

Raia mmoja wa Algeria aliyetambulika kama Nou Mediouni, alikamatwa katika eneo la Kaskazini mwa Uhispania,

Mshukiwa wa pili raia wa Morocco alikamatwa katika eneo la Murcia Kusini mwa nchi.

Kwa mujibu wa duru za serikali, Wote wawili, data yao inafanana na washukiwa wengine wawili waliofanya mashambulizi ya Boston Marathon.

Polisi, wa Ufaransa ndio waliosaidia kuwasaka washukiwa hao.

Al-Qaeda kutoka Kaskazini mwa Afrika ni miongoni mwa wapiganaji wanaoshirikiana na wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.

Kundi hilo lina mizizi yake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mapema miaka ya tisini lakini mnamo mwaka 2007, liliibuka kama moja ya makundi ya wapiganaji wa kiisilamu walio na uhusiano na mtando wa Osama Bin Laden.

Wapiganaji hao wanasema lengo lao ni kueneza sheria za kiisilamu na wanasifika kwa kuteka nyara raia wa kigeni .

Hata hivyo haijabainika ikiwa wawili hao walikuwa na njama ya kufanya mashambulizi.