Burundi yahimizwa kupanga uzazi

Image caption Burundi ina viwango vya juu vya umaskini

Burundi ikiwa ni moja ya nchi masikini sana duniani imetakiwa na shirika la umoja wa mataifa linalo jihusisha na ongezeko la watu duniani kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa ili kupunguza umasikini huo.

Imelengwa kila mwanamke azae watoto wasio zidi watatu katika malengo ya maendeleo hadi mwaka 2025.

Shirika hilo la Umoja wa mataifa limeanzisha kampeini kabambe ya kuwahimiza wananchi kupanga uzazi.

Miongoni mwa masuala yaliyochapishwa na shirika hilo kuonyesha umuhimu wa kupanga uzazi ni kuwa kila mwanamke wa Burundi, kwa uchache ametajwa kuzaa watoto zaidi ya sita inatishia kuiweka nchi hiyo miongoni mwa nchi za Afrika iliyo na msongamano mkubwa zidi wa makaazi.

Burundi ni nchi ndogo iliyo na wakaazi milioni nane waliosongamana katika kilomita mraba elfu ishirini na nane pekee.