160 wathibitishwa kufariki Bangladesh

Maafisa nchini Bangladesh sasa wanasema kuwa watu mia moja na sitini wamefariki baada ya jumba la orofa nane kuporomoka katika viunga vya mji wa Dhaka jana asubuhi.

Makundi ya waokoaji yanajikamua usiku kucha kujaribu kuwaondoa waathiriwa waliokuwa wamkwama katika vifusi. Walikuwa na upungufu wa vifaa vya kuwasidia kupenya katika kuta za saruji na vyuma .

Waokoaji hao wanasema kuwa wamekuwa wakiwasikia waathiriwa waliokwama katika vifusi hivyo wakilia na kuomba kusidiwa.

Jengo hilo lilikuwa na viwanda vichache vya nguo, benki na maduka. Kulikuwa na nyufa katika jengo hilo kabla lipomoromoke hapo jana lakini mameneja waliwaambia wafanyikazi wasitie wasiwasi.

Jamaa za waathiriwa bado wanasubiri kando ya jingo hilo.Zaidi ya watu elfu moja wamejeruhiwa katika tukio hilo. Maafisa wanasema kuwa itachukua siku mbili kumaliza shughuli hiyo ya uokoaji.

Zaidi ya watu elfu moja wamejeruhiwa. Polisi wanasema kuwa wamiliki wa jengo hilowameshtakiwa kwa kosa la kusababisha mauaji.