Polisi wakamata watu Bangladesh

Polisi wa Bangladesh wanasema kuwa wamewakamata wahandisi wawili ambao inasemekana walihusika na jengo la kiwanda liloporomoka mjini Dhaka siku ya Jumatano na kuuwa watu zaidi ya 300.

Wanatuhumiwa kuwa walitoa idhini kwamba jengo hilo ni salama siku moja kabla ya kuporomoka.

Tajiri wa viwanda vya kutengenza nguo kwenye jengo hilo pamoja na meneja wake mkuu piya wamekamatwa.

Watu wanaofanya kazi za uokozi bado wanafukua kifusi kujaribu kuwafikia mamia ya watu ambao wanafikiriwa kuwa bado wamenasa.

Watu kama 26 walinusuriwa Jumamosi huku waokozi wamekuwa wakipenyeza chakula na maji kwa manusuru walionasa ndani ya kifusi.