Seneta Mutula Kilonzo wa Kenya afariki

Taarifa kutoka Kenya zinasema kuwa Mutula Kilonzo, mjumbe wa baraza la senate na waziri wa zamani, amefariki dunia.

Sababu ya kifo chake hakijaelezwa.

Bwana Kilonzo amewahi kuwa waziri wa sheria na maswala ya katiba katika serikali ya kiongozi mstaafu, Rais Mwai Kibaki, na baadae alikuwa waziri wa elimu.

Bwana Kilonzo alichaguliwa kwenye baraza la senate kwa niaba ya chama cha upinzani cha Cord katika uchaguzi mkuu wa mwezi March.