Hoja ya msamaha kwa waasi yarejea Uganda

Image caption Baadhi wanahoji ikiwa muasi Joseph Kony naye pia atasamehewa

Suala la msamaha kwa waasi nchini Uganda hasa wale wa kundi la Lord Resistance Army-LRA- la Joseph Kony pamoja na makundi mengine ya uasi nchini humo laonekana haliishi.

Hii ni kutokana na masuala kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza tangu itangazwe kuwa msamaha haupo tena.

Kuna wanaosema kuwa serikali ilisimamisha msamaha baada ya kuona kwamba haukuzaa matunda yaliyonuiwa ,lakini wengine wanadai kuwa muda wake ulikuwa umeisha.

Hata hivyo sauti zinazidi kusikika nchini humo zikidai urejee kwa vyovyote vile.

Sauti mpya kutaka kurejeshwa msamaha huo kwa waasi ni bunge la taifa.

Tume ya ulinzi ya bunge la taifa imependekeza kifungu cha msamaha kwa waasi kinafaa kirejeswe upya ili kuweza kufanikisha lengo la kifungu hicho ambacho kilisimamishwa kwa muda ikisemekana muda wake iliisha.

Mbunge Simon Mulongo ni makamu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya bunge anafafanua.

Image caption Akina mama na watoto wameathirika sana kutokana harakati za waasi Uganda

Nayo makundi ya kiraia mfano kama la viongozi wa kidini wa eneo la kaskazini maarufu kama kundi la vingozi wa kidini kutoka Acholi linalopigania amani linataka saana msamhana huo, hoja hiyo ikitiliwa mkazo na makamu mwenyekiti wake Sheikh Musa Khalili ambae pia ni kadhi mkuu wa Gulu.

Inasemekana watoto zaidi ya elf 11 ndio walinufaika na msamaha huo ambao uliwekwa na serikali ya sasa ya Rais Museveni. Kwa hivyo wazee kutoka kaskazini mwa Uganda walikuwa na ombi

Lakini msemaji wa jeshi la Uganda kanali Felix Kulajiye anasema kwa kuelewa kwake msamaha bado upo.

Jamil Mukulu ni kiongozi wa kundi la uasi la Allied democratic Front ambalo linaendesha harakati zake Mashariki mwa Kongo na limekuwa likishambulia Uganda kila mara upande wa Kasese.

Swali ni je hata muasi Kony anaweza kusamehewa chini ya msamaha huu wa Rais?

Katika mmantiki hiyo kuna baadhi ya wanawake ambao wamerejeshwa juzi kutoka Kongo mkiwemo wawili wakidai kuwa ni wake wa muasi Kony.Haijulikani ikiwa nao watapewa msamaha wa rais .