Picha za Washukiwa wa mashambulizi Benghazi

Shirika la ujasusi la Marekani FBI limetoa picha za watu watatu wanaosemekana kuwa katika makao ya ubalozi wa Marekani mjini Beghazi wakati iliposhambuliwa mwaka jana.

Shirika hilo linasema kuwa picha hizo zinaweza kutoa taarifa muhimu kuhusu waliofanya shambulizi hilo. Hata hivyo haijasema ikiwa ni washukiwa.

Shambulizi hilo lililosababisha mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya lilifanyika tarehe 11 mwezi Septemba

Wanarepublican katika bunge la Congress wanaendelea kuilaumu serikali ya Obama kuhusu hali ya usalama ilivyokuwa kabla ya shambulizi hilo.

FBI sasa linawataka wananchi wa Libya na watu kote duniani kutoa taarifa zozote kuhusu mashambulizi hayo.