Mjumbe maalum wa UN Mary Robinson ziarani Uganda

Image caption Hali Mashariki mwa DRC ingali tete

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la maziwa makuu la Afrika , Mary Robinson anaanza ziara yake Uganda ili kuelewa fika hali halisi ilivyo.

Hii ni sehemu yake ya ziara rasmi katika eneo ambalo limezongwa na mapigano ya kila mara nchini hususan nchini Congo.

Ziara ya mjumbe maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la maziwa makuu nchini Uganda imekuja wakati muhimu kutokana na hali kuwa tete katika eneo hilo.

Kikosi maalum cha kinachoungwa na Umoja wa Mataifa kikiongozwa na majeshi ya Tanzania kinajiandaa kushika doria Mashariki mwa Congo hususan eneo la Goma.

Huku wapiganaji wa M23 wakisikika kutishia kuuteka tena mji wa Goma ambao waliuhama kama sharti la kukaa katika meza moja na utawala wa Kinshasa kuzungumzia manunguniko yao yaliyowafanya kuasi jeshi la serikali.

Llicha ya mazungumao hayo kufanyika baado hakuna la msingi ambalo limefikiwa hadi sasa na majuzi ilidhaniwa kuwa waasi hao wamejiondoa kutoka mazungumzo hayo baada ya kikosi cha kannda kuanza kuwasili Goma.

Rais wa kundi hilo,Betrard Bisimwa alikanusha kuwa kundi lake limeondoka kutoka mazungumzo bali kusema kuwa , baadhi ya wajumbe wake wamerudi nyumbani kuona familia zao.

Lakini matamshi yake yalionekana yakipingana na ya msemaji wa jeshi la kundi hilo,Kanali Vianney Kazarama, ambaye amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa , vijana wake wanajiandaa kupambana kijeshi na kikosi hicho.

Uganda mbali na kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo, pia rais wake,Museveni ni mpatanishi mkuu wa mgogoro huo, jukumu la kuendesha mazungumzo alimtwika waziri wake wa ulinzi Dr Crispus Kiyonga.

Kwa mantiki hiyo mjumbe huyo, anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo sio tu na rais Museveni lakini pia na mwenyekiti wa mazungumzo hayo Dr Kiyonga.

Haijulikani ikiwa ataweza pia kupata wasaa kuwasikiliza wapiganaji wa M23 akiwa hapa kwani kuna baadhi ya wajumbe wake hapa, ila mbali na wapanishi wakuu pia anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo na makundi kadha yasiyo ya kiserikali.

Baadhi ya makundi hayo imeelezwa ni ya akina mama na pia na yale ambayo yanashirikiana na Umoja wa Mataifa na pia yale ya kimataifa.

Ikumbukwe kuwa hivi maajuzi viongozi kadhaa wa mataifa ya kanda ya maziwa makuu walitia saini hati ya kushirikiana ili kuleta amani nchini Congo pamoja na kanda nzima.

Uganda na Rwanda kila mara zimekuwa zikinyoshewa kidole cha kuyaunga mkono kwa hali na mali baadhi ya makundi ya waasi ya mashariki mwa Congo kama vile M23 jambo ambalo viongozi wa nchi hizo , kila mara wamekuwa wakikana.

Kama hatua ya kuonyesha hawana uhusiano wowote na kundi la M23, rais Museveni na Kagame wa Rwanda ni miongoni mwa viongozi waliotia saini, hati hiyo mjini Addis Ababa Ethiopia.

Kuja Uganda, Bi Mary Robinson anatokea Rwanda ambako bila shaka amezungumza na washika dau kuhusu mgogoro wa mashariki mwa Congo.

Baadaye ataelekea Burundi na kisha Afrika Kusini na kukamilisha ziara yake nchini