Gupta:maafisa watano wasimamishwa kazi

Image caption Sherehe za harusi ya familia ya Gupta, Mjini Sun City, Afrika Kusini

Maafisa watano waandamizi katika Afrika ya Kusini wamesimamishwa kazi wakati serikali inachunguza ukiukwaji wa usalama wakati wa harusi ya mojawapo wa familia mashuhuri za India.

Waziri wa sheria alisema maafisa watatu wa polisi nao pia wamekamatwa.

Familia moja tajiri ya India iliruhusiwa kutua kwa ndege yao ya kibinafsi katika kituo cha kijeshi karibu na jiji la Pretoria.

Familia ya Gupta ambayo iliwasafirisha kwa ndege walikwa wa ndoa hiyo mkiwemo wacheza senema wa filamu za Bollywood na maafisa wa serikali;imekanusha kufanya kosa lolote.

Atul, Ajay na Rajesh Gupta ni ndugu inaosemekena wana ushawishi mkubwa katika Afrika ya Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu wachache mnamo mwaka 1994.

Maslahi yao ya biashara yanahusu maadini,usafiri wa ndege,teknolojia na vyombo vya habari.

Mnamo siku ya Alkhamisi ilitangazwa pia kua ubalozi wa India utachunguzwa kuona kama ulikiuka haki za kibalozi kuhusiana na harusi hiyo.

Waandishi wa habari wanasema kashfa hiyo imesababisha hasira nyingi nchini Afrika ya Kusini na wabunge wa wa upionzani na jumuiya ya wafanyakazi Cosatu imehimiza ufanyike uchunguzi kamili wa bunge..

Gupta wasikitika

Waziri wa sheria Jeff Radebe alihutubia mkutano wa waandishi w ahabari mjini Pretoria siku ya Ijumaa akiwa pamoja na mawaziri na maafisa kadhaa waandamizi wa usalama.

Image caption Maharusi wa familia ya Gupta wafunga ndoa

Amesema tume hiyo ya uchunguzi imepewa siku saba kukamilisha uchunguzi na kutoa ripoti yao kwa baraza la mawaziri kueleza ilikuaje ndege ya kibinafsi ikiwa na wageni walikwa 200 wa familia ya Gupta kutoka India ilikwenda kutua katika kitupo cha wanahewa cha AFB) Waterkloof.

Familia ya Gupta ilisema imesikitishwa sana "taarifa potofu zinazoendelea kutolewa kuhusu harusi hiyo. " Serikali nayo "imeshtushwa na ukiukwaji wa kanuni za usalama na kupuuzwa kabisa utaratibu wa kutia idhini kwa ndege kuruka ama kutua katika kituo cha kijeshi ambacho ni muhimu kwa taifa" alisema Bwana Radebe.

Mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa India alipeleka ombi la kutaka idhini ya ndege hiyo kutua,moja kw amoja kwa kikosi cha kijeshi.

Mnamo siku ya Jumaanne ilielekea wageni waalikwa wa harusi hiyo walisindikizwa na polisi kwa mji wa starehe wa Sun City kwa harusi ya mpwa wa nduguwa Gupta; Vega Gupta mwenye umri wa miaka 23.,

Kesi ya jinai imefunguliwa kwa kua magari yalitumia nambari na vimuri vya bandia alisema waziri wa sheria.

Maafisa watatu wa polisi walikmatwa kutokana na kuhusika katika tukio hilo .