Mwendesha mashtaka auwawa hadharani Pakistan

Image caption Polisi wanakagua gari la Chaudhry Zulfiqar aliyepigwa risasi

Watu wenye silaha wamemuua mwendesha mashtaka maalum anayechunguza kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Benazir Bhutto katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad. Bi Bhutto aliuwawa katgika shambulio la bomu mnamo mwaka 2007.

Chaudhry Zulfiqar amepigwa risasi na watu waliopanda pikipiki alipokuwa akiendesha gari kwenda mahakamani,na alifariki baadaye hospitalini.

Alikuwa pia mwendesha mashtaka mkuu katika kesi iliyohusika na shambulio la wanamgambo la mwaka 2008 mjini Mumbai lililowaua watu 166. Polisi hawakutoa maelezo yoyote kuhusu sababu za shambulio hilo.

Aliekua Waziri Mkuu wa Pakistan Pervez Musharraf ameshtumiwa kwa kushindwa kutoa ulinzi wa kutosha kwa Bhutto wakati wa kifo chake.

Bwana Musharraf, ambae amerejea hivi majuzi tu nchini Pakistan baada ya kuishi ng'ambo yuko chini yha kifungo cha nyumbani wakagti madai dhidi yake yanachunguzwa. Anakanusha madai hayo. w

Hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyepatgikana na hayia kwa mauaji ya bi Bhutto.

Msemaji wa hospitali amesema Chaudhry Zulfiqar alipigwa zaidi ya risasi saba mwilini na kichwani.

Mwanamke mmoja mmpita njia pia alifariki baada ya kugongwa na gari la Chaudhry Zulfiqar baada ya dereva kupoteza udhbiti wa usukani.

Washambualiaji hao baadae walitoroka.

Magazeti ya Pakistan yamearifu kuwa wanasheria katika Islamabad na Rawalpindi wameamua kugoma ili kuonyesha malalamiko yao dhidi ya mauaji hayo.