Mpaka wa Afghanistan na Pakistan kumoto

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya janga jipya liloanza upande wa Pakistan kwenye mpaka wake na Afghanistan, mpaka wenye mzozo.

Katika miezi michache iliyopita kumezuka mapigano tena mpakani baina ya wanajeshi wa Afghanistan na Pakistan.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR, limesema kuwa watu zaidi ya 70,000 wamekimbia majumbwani mwao tangu kati ya mwezi wa March.

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema serikali yake katu haitatambua mpaka huo ambao uliwekwa mwaka wa 1893 na wakoloni Waingereza - mpaka uloitenga maeneo ya makabila fulani ambayo kijadi yalikuwa pamoja.