Aliyemtumikia Gaddafi hakubaliki sasa

Libya imepitisha sheria itayopiga marufuku maafisa kutoka serikali ya hayati Kanali Gaddafi kushika wadhifa sasa.

Sheria hiyo imepitishwa na Baraza la Taifa juma moja baada ya wanamgambo waliodai sheria hiyo walipoanza kuzingira wizara za sheria na mashauri ya nchi za nje.

Walisema hawataondoka hapo hadi sheria hiyo ipitishwe.

Ilipokubaliwa walianza kusherehekea.

Sheria hiyo itawaathiri maafisa waandamizi wa serikali pamoja na waziri mkuu, Ali Zeidan.