Morinho kuifufua Chelsea asema Lampard

Frank Lampard
Image caption Frank Lampard

Frank Lampard amesema anaamini kuwa Jose Mourinho anaweza kuandikisha matokeo mema kwa mara nyingine kama alivyofanya wakati alipoteuliwa kocha wa Chelsea kwa mara ya kwanza ikiwa atarejea tena.

Ripoti zinasema kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 50, anakaribia kuihama klabu ya Read Madrid, kuchukua mahala ka kaimu kocha wa klabu hiyo kwa sasa Rafael Benitez.

Lampard, ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi la Chelsea siku ya Alhamisi, ameiambia BBC kuwa, haiwezekani kwa kocha huyo kurejea na kutulia na kutegemea rekodi yake ya zamani.

Amesema, ikiwa atarejea kwa mara nyingine, Chelsea huedna ikaibuka na ushindi mkubwa msimu ujao.

Akiwa Chelsea, Morinho alishinda vikombe sita katika kipindi cha miaka mitatu, viwili vikiwa vya ligi kuu ya premier, lakini alijiuzulu Septemba mwaka wa 2007, baada ya uhusiano wake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Ambramovich kusambaratika.

Morinho alijiunga na klaby ya Inter Millan Juni mwaka wa 2008, ambako alishinda vikombe zaidi, moja la Bara Ulaya na vingine viwili vya ligi kuu ya Serie a.

Image caption Jose Morinho

Mwaka wa 2010, alijiunga na Klabu ya Real Madrid na mwaka wake wa kwanza alishinda kombe la Copa del Rey kabla ya kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu ya La Liga kutoka kwa vigogo wa soka nchini Uhispania Barcelona.

Kurejea kwa Mourinho, kunakisiwa kuwa sababu kubwa ya Kandarasi ya Frank Lampard kuongezwa kwa mwaka mmoja zaidi.

Wiki iliyopita Lampard aliandikisha historia ya kuwa mchezaji wa Chelsea aliyefunga idadi kubwa zaidi ya magoli, baada ya kuvunja rekodi iliyowekwa na Tambling ya magoli 202.

Lampard amefunga magoli 203.