Sheria ya wanawake Afghanistan yapingwa

Wabunge wa Kiislamu wenye msimamo mkali nchini Afghanistan wamezuia mjadala wa bunge kuhusu sheria ya kuwalinda wanawake na dhulma.

Mjadala huo ulikwama baada ya dakika 15 katika mabishano makali, pale wanasiasa wasiotaka mabadiliko walipotaka sheria hiyo ifutwe - sheria iliyoanzishwa na Rais Hamid Karzai miaka mine iliyopita bila ya idhini ya bunge.

Walimshutumu Bw. Karzai kwamba amekiuka sharia za Kiislamu.

Mamia ya watu, hasa wanaume, wamefungwa kufuatana na sheria hiyo ambayo inapiga marufuku utumiaji nguvu dhidi ya wanawake, ndoa za watoto na ndoa za lazima.