Ubaguzi kwa Waislamu waongezeka

Shirika la Uingereza la mchanganyiko wa dini mbali-mbali linasema jamii zimeingiwa na uoga tangu kuchinjwa kwa mwanajeshi wa Uingereza na Waislamu wenye siasa kali katika barabara ya mjini London.

Shirika hilo, Faith Matters, limesema mashambulio yameongezeka sana tangu kuuwawa kwa mwanajeshi huyo siku ya Jumatano.

Linasema limearifiwa visa zaidi ya 162 vya ubaguzi dhidi ya Waislamu katika siku mbili - kutoka misikiti kushambuliwa hadi matusi.

Viongozi wa Kiislamu wa Uingereza wamelaani vikali mauaji ya mwanajeshi huyo.