Mtoto alianguka kwa bahati mbaya China

Image caption Mtoto huyu alipewa jina la 59 anaendelea kupokea matibabu

Mtoto mchanga aliyeokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka nchini China, alianguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya, mamake mtoto huyo amesema.

Mama huyo ambaye bado hajatajwa jila lake, aliambia polisi kuwa alijifungua mwanawe akiwa chooni na kuwa mtoto huyo aliteleza na kuanguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya

Mama huyo anaripotiwa kuangua kilio cha mwanawe , licha ya kuwa hakukubali kuwa ni mwanawe hadi baadaye.

Mtoto huyo anapokea matibabu hospitalini baada ya kuokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka. Bomba hilo lilikatwa kwa ustadi baada ya majirani kusikilia kilio cha mtoto huyo mjini Jinhua Jumamosi.

Shirika la habari la Zhezhong, lilisema kuwa mamake mtoto huyo mwenye umri wa miaka 22, aliambia polisi kuwa hangeweza kumudu gharama ya kuavya mimba. Hajaolewa na aliiweka mimba yake kuwa siri kubwa.

Alisema kuwa alijaribu kumzuia mtoto wake kuanguka baada ya kujifungua kwa ajali akiwa hospitalini lakini alianguka ndani ya bomba. Hata hivyo alimweleza mpangaji wake kulingana na shirika la habari la Xinhua.

Mama huyo alisema hakuwa na uwezo wa kumlea mwanawe kwa hivyo hakuambia yeyote kuwa ni mwanawe. Hata hivyo baadaye alijitambulisha na kuambia polisi ni mwanawe baada ya kuokolewa kwake.

Image caption Bomba aliloanguka ndani mtoto huyo

Polisi wanachunguza ikiwa tukio hilo lilikuwa la ajali au kilikuliwa kitendo cha maksudi.

Mtoto huyo alipatikana ndani ya bomba lenye urefu wa nchi nne

Alipata majeraha madogo kichwani na mikononi lakini anaendea kupata matibabu.

Kisa hicho kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya China huku baadhi wakisema kuwa mtoto huyo alikuwa ametupwa na mamake kwa maksudi.

Sheria za China za kupanga uzazi ni kali mno huku familia ikiruhisiwa kuzaa mtoto mmoja pekee na wazazi wanaweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini ikiwa watapatikana na hatia ya kupata zaidi ya mtoto mmoja.