Al-Qaeda wana silaha za kemikali Iraq

Wakuu wa Iraq wanasema wamegundua njama ya al-Qaeda kutaka kutumia silaha za kemikali nchini Iraq na kuzisafirisha kwa magendo hadi Ulaya na Marekani.

Msemaji wa wizara ya ulinzi, Mohammad al-Askari, alisema idara ya usalama ya jeshi imegundua karakana tatu za kutengeneza kemikali hizo, pamoja na kemikali ya kuharibu neva.

Bwana al-Askari aliiambia televisheni ya Iraq kwamba wanaume watano walikamatwa baada ya kuchunguzwa kwa miezi mitatu.

Wote walikiri makosa, alisema.