Adhabu dhidi ya Banguora idumishwa:CAS

Image caption Ismael Bangoura

Rufaa iliyowasilishwa katika mahakama ya kimataifa ya michezo CAS na mchezaji wa Guinea Ismael Bangoura, kupinga adhabu aliyopewa ya kutocheza mechi yoyote kwa muda wa miezi minne imefuliwa mbali.

Mzozo huo ulikuwa unahusiana na sakata ya uhamishwa ya mchezaji huyo.

Mahakma hiyo pia, pia imeipiga marufuku klabu ya Nantes, iliyopandishwa daraja dhidi ya kusajili mchezaji yeyote katika awamu mbili zijazo za kuwasijili wachezaji wapya.

Klabu hiyo ya Nantes na Bangoura, vile vile wameshurutishwa kulipa dola milioni nane nukta nane tatu kwa klabu ya Al Nasr inayoshiriki ligi kuu ya Milki za kiarabu.

Mahakama hiyo ya CAS, iliagiza kuwa hukumu iliyotolewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, kuwa Bangoura ana hatia ya kuvunja mkataba wakati alipokihama klabu ya Al Nasr na kujiunga na Nantes mwaka wa 2012 idumishwe.

Hata hivyo mahakama hiyo ilifutilia mbali ombi la Al Nasr la kutaka fidia hiyo kuongezwa zaidi.

Bangoura, ambaye aliwahi kuichezea Dynamo Kiev na Stade Rennes, alijiunga na Al Nasr, kwa mkataba wa miaka minne Septemba mwaka wa 2010.

Mwanzo wa mwaka wa 2012, aliwakilisha taifa lake katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika, baada ya kupata idhini ya klabu yake, lakini alipoteza nafasi yake baada ya Al Nasr kumsajili mchezaji mwingine kuchukua mahala pake.

Bangoura kisha akajiunga na Nantes, ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja ya pile na alisajiliwa na klabu ya Umm Salal YA Qatar, kwa mkopo Septemba mwaka huo.