Musharraf akamatwa na polisi

Image caption Polisi waliokwenda kumkamata Pervez Musharraf

Polisi nchini Pakistan wamemkamata kiongozi wa zamani wa kijeshi wa nchi hiyo Pervez Musharraf, kuhusiana na mauaji ya gavana wa jimbo moja mwaka wa 2006.

Polisi kutoka mji wa Balochistan, walisafiri hadi nyumbani kwake rais huyo wa zamani mjini Islamabad, na kumfungulia mashtaka ya mauaji ya kiongozi wa eneo la Balochistab, Akbar Bugti.

Kiongozi huyo wa zamani Amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani kwa muda wa mwezi mmoja uliopita, baada ya kupatikana na hatia kutumia madaraka yake vibaya wakati alipokuwa kiongozi wa taifa hilo.

Hata hivyo Bwana Musharaff aliachiliwa kwa dhamana lakini ombi lake la kutaka pia kuachiliwa kwa dhamana kuhusiana na mauaji hayo ya kiongozi wa Bolochsitan lilikataliwa mapema wiki hii.