Mshukiwa wa ugaidi auawa Kenya

Image caption Mji wa Garissa ndio umekuwa kitovu cha mashambuzli ya kuvizia yanayofanywa na wapiganji wa Al Shabaab

Mshukiwa wa ugaidi amepigwa risasi na kuuawa mjini Mombasa Pwani ya Kenya.

Mshukiwa huyo alipigwa risasi baada ya kusita kujisalimisha kwa polisi. Alipatikana na maguruneti na zaidi ya bunduki mbili akiwa na risasi miambili nyumbani kwake mtaa wa Kisauni.

Mkuu wa polisi mjini humo Aggrey Adoli anasema kuwa mshukiwa alikuwa anapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Mombasa na Nairobi.

Tukio hilo linakuja wiki moja baada ya watu sita kuuawa katika shambulizi la kigaidi lililofanya dhidi ya kanisa mjini Mombasa.

Polisi wamekuwa wakiwalaumu wapiganaji wa kiisilamu wa kundi la Al Shabaab kwa kufanya mashambulizi kama haya mara kwa mara nchini Kenya.