Wabunge 4 wa upinzani wakamatwa Arusha

Image caption Moja ya eneo ambalo lilikumbwa na shambulizi la bomu mjini Arusha

Vurugu zimeendelea mjini Arusha ambapo jana polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kudhibiti mikutano ya hadhara kufuatia polisi kutangaza kutokuwepo kwa mikusanyiko ili kuimarisha usalama kufuatia mlipuko wa pili uliotokea mjini Arusha, baada ya mtu asiyejulikana kurusha bomu katika mkutano wa kisiasa

Wabunge wanne wa CHADEMA jana wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko bila kibali ambapo viongozi hao wa chama cha upinzani cha CHADEMA walikusanyika katika eneo kulikotokea mlipuko wa bomu la viwanja vya Soweto kwa malengo ya kutaka kufanya mkutano

Wabunge wanaoshikiliwa na polisi ni Tundu Lissu,Said Arfi , Joyce Mukuya mustafa Akoonay ambapo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kukamatwa kwa wabunge hao.

Hata hivyo kuna madai kuwa baadhi ya viongozi wengine wa chama cha Chadema wanasakwa na POLISI, wabunge hao wanatuhumiwa kuwahamasisha wafuasi wao kuwashambulia polisi kwa mawe wakati walipotakiwa kuondoka katika viwanja hivyo kwa hiari.

aidha polisi pia imekitaka chama cha CHADEMA kuwasilisha kile ilichodai kuwa ni ushahidi wa mtu aliyehusika na urushaji wa bomu hilo

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, inadaiwa kuwa bomu lililorushwa katika mkusanyiko huo lilitengenezwa nchini China. Kiongozi wa harakati dhidi ya tukio hilo Paul Chagonja amesema polisi wako tayari kupokea ushahidi kutoka kwa viongozi hao wa kisiasa wanaodai wana taarifa za mtu huyo aliye husika

Jana pia kumetokea vurugu kwa kile kilichodaiwa ni baada ya polisi kuzuia mkutano mwingine wa hadhara uliokuwa ukilenga kutaka kufanya ibada ya mazishi.