Uhasimu katika kundi la Al Shabaab

Image caption Baadhi wa viongozi wa Al Shabaab wamekanusha madai kuwa kuna migawanyikokatika kundi hilo

Makabiliano yametokea kati ya mirengo hasimu katika kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia Al Shabaab karibu na mji wa Pwani wa Brava.

Wapiganaji sita wakiwemo raia wawili wa kigeni waliuawa katika makabiliano makali ya kufyatuliana risasi .

Hata hivyo, Al-Shabab limekanusha kuwepo malumbano kati ya viongozi wa kundi hilo.

Ikiwa hili litathibitishwa, hii itakuwa mara ya kwanza kuwepo kutolewana kati ya mirengo ya kundi hilo lwnye uhusiano na al-Qaeda tangu kluanza kwa harakati zake mwaka 2006.

Mnamo Jumatano takriban watu 15 waliuawa kwenye shambulizi lililofanywa na al-Shabab dhidi ya ofisi za Umoja wa mataifa mjini Mogadishu.

Wapiganaji wake walilipua bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gali lililokuwa limeegeshwa kando ya lango kuu la ofisi za UN.

Wenyeji wamesema kuwa hali ni tete katika mji wa Berava kufuatia makabiliano makali kati ya makundi hasimu ya wapiganaji wa kiisilamu

Al-Shabab imegeuza mji huo na kuwa kama ngome yake kuu baada ya kupotyeza uthibiti wa maadhi ya miji waliyokuwa wameiteka.

Sababu kuu ya makabiliano hayo haijulikani lakini kumekuwa na mzozo kuhusu mamlaka kati ya al-Shabab ikimhusisha kiongozi wake Ahmed Abdi Godane na msemaji wa kundi hiloMuktar Ali Robow.

Bwana Robow anasemekana kuwa na msimamo wa kadri kuliko bwana Godane, na anapinga uhusiano kati yao na al-Qaeda.

Hata hivyo, msemaji wa al-Shabab Ali Dheere alipuuza madai hayo ya makabiliano mjini Brava na kuyataja kuwa "propaganda" na uongo mtupu.

Aliongeza kuwa kundi hilo lina mshikamano.