Makao ya chama kikuu yavamiwa Misri

Image caption Maandamano dhidi ya rais Morsi watu wakimtaka aondoke mamlakani

Waandamanaji wanaopinga serikali nchini Misri, wamevamia makao makuu ya chama tawala cha Muslim Brotherhood mjini Cairo.

Inaarifiwa wamepora mali iliyokuwa kwenye ofisi hizo katika mji wa Moqattam wakitupa baadhi ya vitu nje ya madirisha kabla ya kuiteketeza ofisi yenyewe.

Rais Mohammed Morsi ni rais wa chama hicho cha kiisilamu chenye ushawishi mkubwa.

Awali, vuguvugu la upinzani lililoandaa maandamano hayo, ambayo yameshuhudia mamilioni ya watu wakijitokeza kuandamana nchini Misri, wametoa makataa kwa rais Morsi hadi Jumanne ajiuzulu.

Taarifa iliyotolewa na kundi hilo, Tamarud au (waasi) ilisema kuwa bwana Morsi huenda akakumbana na raia wasiotii sheria kama njia ya kumuonyesha kuwa wanampinga ikiwa hataondoka mamlakani na kuruhusu uchaguzi kufanyika.

Mamilioni ya watu walihudhuria maandamano, nchini kote Jumapili kumtaka Morsi kuondoka mamlakani.

Pande zote husika zilishangazwa na maandamano yanayofanywa dhidi ya Morsi.

Upinzani ni muungano wa vyama vingi, vikiwemo vianvyomuunga mkono rais aliyeng'olewa mamlakani Mubarak pamoja na watu waliojitolea maisha yao kumuondoa mamlakani.

Changamaoto kwano ni kutafuta njia ya kuendwel;eza maandamno yenyewe hadi wanachokitaka kitakapotimia.

Masemaji wa rais Morsi ameitisha mkutano kati ya pande husika.

Kwa hilo kufanikiwa, rais atahitajika kujitolea na kukubali matakwa yao, ikiwemo hata kufanyia katiba marekebisho.

Hakuonyesha dalili za kutaka mwafaka na wanaompinga, alipokuwa anatoa hotuiba yake wiki jana.

Kwa waandamanaji, wanataka aondoke mamlakani kwa kuitisha uchaguzi wa mapema. Kwa sasa vurugu inaonekana zitaendelea kwa muda.