"Nelson anapata nafuu", Zuma

Image caption Watu wakituma kheri njema ya nafuu kwa Madiba

Nelson Mandela anaendelea kupata nafuu, licha ha afya yake kuendelea kuwa mbaya. Hii ni kwa mujibu wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, baada ya kumtembelea hospitalini. Rais huyo wa zamani amelazwa hospitalini ambapo anamatatizo ya kupumua.

Rais Zuma amewaomba raia wa Afrika Kusini kuendelea kuonyesha mapenzi yao kwa Mzee Madiba.Kiongozi wa jamii ya Thembu, Mfalme Buyelekhaya Dalindyebo aliambia shirika la habari la AFP kwamba Mandela alikua na fahamu alipomtembelea hospitalini.

Wiki jana Rais Zuma alikanusha taarifa kwamba Mandela alikuwa hali mahututi. Shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini alifungwa jela miaka 27 na kuachiwa huru mwaka 1990. Alichaguliwa Rais mwaka wa 1994 na kuhudumu kwa muhula mmoja pekee.