Msanii Chiwoniso Maraire afariki dunia

Image caption Chiwoniso alisifika sana mapema miaka ya tisini

Mmoja wa wanamuziki mashuhuri sana nchini Zimbabwe Chiwoniso Maraire, amefariki akiwa na umri wa miaka 37 kwa mujibu wa meneja wake.

Album ya Chiwoniso kwa jina 'Ancient Voices' ilimpa sifa tele katika ukumbi wa kimataifa mapema miaka ya 1990.

Alicheza ala ya muziki ijulikanayo kama Mbira, ambayo wanaume pekee ndio wanaruhusiwa kuicheza nchini Zimbabwe.

Anasemekana alifariki kutokana na homa ya mapafu, mwaka mmoja tu baada ya aliyekuwa mumewe, Andy Brown, ambaye pia alisifika kwa muziki wake nchini Zimbabawe kufariki. Walikuwa na watoto wawili.

Chiwoniso aliyekuwa mwanawe mwanamuziki mashuhuri nchini humo ambaye pia alisifika kwa kucheza ,Mbira Dumisani Maraire, alisomea katika chuo kikuu cha Zimbabwe.

Alizaliwa nchini Marekani mwaka 1976, kabla ya kuhamia nchini Zimbabwe akiwa na umri wa miaka saba.

Je ulimfahamu Chiwoniso Maraire? Una kumbukumbu zipi kumhusu? Unaweza kutuleezea kupitia ukurasa wetu wa facebook bbcswahili.